Maswali na majibu

Wese ni mfumo wa teknolojia unaowezesha watoa huduma za usafiri kununua mafuta sasa na kulipa baadae bila riba kila siku.

Unaweza kujisajili na Wese kwa kupitia wakala kwa kutoa taarifa zinazohitajika na kwa kupakua programu ya Wese au kwa kupiga *149*65#.

Ili kujiunga na Wese, unahitaji kujisajili kupitia wakala kwa kutoa taarifa zako binafsi.

NDIYO, Wese inapatikana kwenye App Store pamoja na Play Store.

Ndio, Wese inapatikana katika mikoa mingine tofauti na Dar es Salaam.

Jisajili kwa wakala, kisha weka kiasi ulichonacho kupitia mtandao wako wa simu, Wese itazidisha mara mbili ya kiasi hicho na kituo cha mafuta kitakupa mafuta yenye thamani ya jumla kuu kwa matumizi yako ya siku.

Wakala, anaweza kuwa mtu yoyote ambaye ana nia ya kutengeneza kipato cha ziada, kupitia kuweka pesa kwenye wese ambazo zinaweza kutumiwa na wanachama wake na kupata kamisheni ya matumizi ya kila siku ya wanachama.

Urejeshaji wa pesa lazima ufanyike kabla ya saa sita kamili (06:00) usiku, ambayo inamaanisha wakati wowote ndani ya siku hiyo hiyo.

Ukishindwa kulipa siku hiyo hiyo, utahitajika kulipa adhabu na gharama za huduma wakati kulipia.

HAKUNA kikomo cha miamala kwa siku, mradi tu uko ndani ya vigezo na masharti ya Wakala.

Ofisi za Wese zinapatikana Makumbusho, Mwanga tower ghorofa ya 13.

Hakuna kikomo kwa kiasi cha matumizi.

Ndio! unaweza kujiandikisha kwa wakala zaidi ya mmoja.

Kama mteja huwezi kutumia huduma kupitia kwa mawakala tofauti kwa wakati mmoja, itakulazimu kulipa mkopo wa kwanza kabla ya kuchukua mkopo wa mwingine.

Wese ni kampuni iliyosajiliwa chini ya Brela, na kwa ushirikiano na Benki.

Kama mwanachama unaweza kununua mafuta na kulipa baadae bila riba siku hiyo hiyo, bila hitaji la karatasi au idhini kutoka kwa wahusika wengine.

Ikiwa mfumo haufanyi kazi tafadhali wasiliana na dawati la watoa huduma kwa wateja.

Ili kupata maelezo zaidi kuhusu Wese, tafadhali tembelea tovuti yetu rasmi au wasiliana na timu yetu ya masoko kupitia njia zilizotolewa.

Ili kutatua changamoto, wasiliana na dawati letu la watoa huduma kwa wateja au tembelea kurasa zetu za mitandao ya kijamii.