Maswali na majibu

Wese ni mfumo wa teknolojia unaowezesha watoa huduma za usafiri kununua mafuta sasa na kulipa baadae bila riba kila siku.

Mfumo wa Wese huwawezesha madereva kupata mafuta kwa utaratibu wa "Nunua Sasa Lipa Baadaye". Dereva lazima asajiliwe na wakala ili kutumia huduma hii (Vigezo na Masharti Kuzingatiwa).

Unaweza kuwa wakala kwa kupakua mfumo wa wese kutoka App Store na Google play. Tumia namba yako ya simu kujisajili, nunua kiasi cha mafuta unachohitaji, kisha ongeza wanachama wako na uanze kutengeneza kipato.

Mtu yeyote mwenye mtaji na wanachama walio tayari kujiunga na Wese anaweza kuwa wakala. Vigezo na masharti kuzingatiwa.

Unaweza kufanya miamala na kujisajili kwenye Wese kwa kutumia mtandao wowote wa simu, iwe Vodacom, Tigo, Airtel, TTCL au Halotel.

Kiasi cha chini cha kuanza kufanya biashara kama wakala ni Tsh 100,000/= (shilingi laki moja tu).

Hakuna ada za usajili kabisa si kwa wakala wala mwanachama.

Unaweza kusajili wanachama kwenye mfumo kwa kujaza taarifa zinazohitajika kama vile jina, namba ya simu n.k.

Hakuna kikomo cha idadi ya wanachama ambao unaweza kuwasajili kwenye akaunti yako.

Mwanachama akishindwa kulipa deni lake siku hio hio, ataadhibiwa na kutakiwa kulipa nyongeza ya asilimia 4% ya kiasi alichotakiwa kulipa.

Kama wakala wa Wese, utaweza kupata kipato cha ziada kupitia kamisheni kwa kufanya biashara kwenye mfumo huu.

Mawakala hupata kamisheni kwa kila lita ya mafuta inayonunuliwa na kulipwa kupitia benki mshirika kwenda kwenye namba au akaunti zao za malipo.

Fedha za Wese zipo chini ya uangalizi wa benki mshirika ambayo inashughulikia masuala yote ya kifedha, fedha zote ziko katika mikono salama.

Hakuna kikomo cha mara ngapi unaweza kutoa pesa kutoka kwenye akaunti yako. Lakini huwezi kutoa kiasi chochote chini ya Tsh. 20,000. Vigezo na masharti kuzingatiwa.

Ndio, uwaweza kutoa mtaji wako baada ya siku 28 kutoka siku uliyoweka . Vigezo na masharti kuzingatiwa.

Ili kutatua changamoto yako wasiliana na dawati letu la huduma kwa wateja au tembelea kurasa zetu za mitandao ya kijamii.

Ndio, unaweza kusitisha usajili wako kama wakala kwa kufuata maelekezo ndani ya programu yako.