Vigezo na masharti

i) Wakala lazima apakue Programu ya Wakala wa WESE na afuate utaratibu wa kujisajili ili aweze kufanya biashara kwenye mfumo wa WESE.

ii) Wakala lazima awe na salio la mafuta lenye thamani isiyopungua TZS 100,000/= ili kuanza kufanya biashara kwenye mfumo wa WESE.

iii) WESE itamuongezea wakala mafuta yenye thamani sawa na kiasi alichonunua. Hii itafanya jumla ya mtaji wa mafuta kuwa mara mbili ya alivyonunua wakala husika.

iv) Wakala amepewa uwezo wa kusajili kikundi cha madereva wa usafiri wa kibiashara anaowafahamu (bodaboda, bajaj, teksi, daladala na mabasi) katika jamii. Hivyo basi, wakala atabeba dhamana ya madereva aliowasajili.

v) Madereva waliosajiliwa na wakala wanaweza kujaza mafuta kwenye vituo washirika wa WESE nchini kote kwa kununua sasa na kulipa baadaye. Mda wa mwisho wa kurejesha ni kabla ya saa sita kamili (06:00) usiku. Isipokuwa, dereva akijaza mafuta zaidi ya lita 50 kuanzia saa kumi na mbili jioni na kabla ya saa sita kamili usiku, atapaswa kulipa ndani ya masaa thelathini (30) yatakayohesabiwa kuanzia saa kumi na mbili jioni.

vi) Mawakala hupata kamisheni ya papo hapo kwa kila lita inayotumika kutoka kwenye akaunti yake.

vii) Mawakala wanaweza kutoa mapato, uwekezaji wa ziada, au kughairi uwekezaji wakati wowote. Vigezo na Masharti kuzingatiwa.

viii) Muda wa chini wa biashara ni siku ishirini na nane (28) na notisi ya uondoaji wa mtaji ya masaa sabini na mbili (72) inahitajika ili kuruhusu madereva walio chini ya akaunti, muda wa kutosha wa kujisajili kwa mawakala wengine.

ix) Watumiaji wabaya(wasiolipa kwa wakati) watatozwa ada ya muamala na usimamizi mara moja (1%) pamoja na malipo ya 3% kwenye salio ambalo hawajalipa kila siku kihesabu.

x) Baada ya kukusanya malipo ya adhabu kwa marejesho yaliyo zidisha muda, Wakala ana haki ya kupata 60% ya marejesho.

xi) Wakala anaweza kufunga akaunti yake (kipindi cha huduma iliyosimamishwa), Kitendo cha kufunga kitawasilishwa kwa watumiaji wote kupitia ujumbe wa app na ujumbe mfupi.